Asanteni nyote kwa kuwa sehemu ya "MTANDAO WA ZINDUKASASA" kama watembeleaji, wasomaji na wachangiaji kwa mwaka mzima wa 2016. Tunawatakia kheri katika msimu huu wa sikukuu na mwaka mpya wa 2017.
ZINDUKA SASA BLOG
Saturday, December 24, 2016
Tuesday, December 13, 2016
VISABABISHI VYA KISUKARI
Hujambo rafiki?
KISUKARI: Kula sukari nyingi hakusababishi kisukari bali kula vyakula vya wanga na mafuta kwa wingi huchangia kuongeza uzito ambao ni hatari ya kupata kisukari!
Asante sana kwa kututembelea.
FAIDA YA FIGO MWILINI NA VITU VINAVYOIATHIRI
Hujambo rafiki?
FIGO:Kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu, kusaidia kuhifadhi na kudhibiti kiwango cha maji na madini mwilini zote ni baadhi ya kazi za figo.
FIGO: Matumizi mabaya ya dawa hasa za maumivu, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi ni baadhi ya visababishi vya ugonjwa wa figo, chukua hatua.
Asante sana kwa kututembelea.
FIGO:Kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu, kusaidia kuhifadhi na kudhibiti kiwango cha maji na madini mwilini zote ni baadhi ya kazi za figo.
FIGO: Matumizi mabaya ya dawa hasa za maumivu, uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi ni baadhi ya visababishi vya ugonjwa wa figo, chukua hatua.
Asante sana kwa kututembelea.
NAMNA YA KUZUIA TEZI DUME
Hujambo rafiki?
Tezi dume inaweza kuzuilika kwa kula vyakula vyenye madini ya Zinc kwa wingi kama samaki, pweza, spinachi, mbegu za maboga na matikiti maji.
Asante sana kwa kututembelea.
Tuesday, November 22, 2016
MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.
Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye matandao(blog) wetu wa zinduka sasa tujifunze kuhusu
MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.
- KUWAPA JOTO. Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia kitalu ( mduara) unaoweza kutengenezwa kwa kutumia mbao na karatasi ngumu na kuweka chanzo cha joto ndani.
- UTOSHELEVU WA JOTO. Ufahamu utoshelevu wa joto kwa kuangalia tabia ya vifaranga wanapokuwa ndani ya Kitalu.
Mfugaji unatakiwa kufuatilia vifaranga kwa karibu ili kutambua kama hali ya joto iliyopo inawafaa au laaah. Ufuatiliaji wa karibu husaidia kuchukua hatua mapema kama marekebisho yatahitajika.
Kutegemeana na jinsi utakavyowaona vifaranga, fanya marekebisho mapema kabla madhara hayajatokea kwa vifaranga wako.
Katika majuma 4 au 5 ya kwanza vifaranga huhitaji joto usiku na mchana na katika majuma 3 yanayofuata joto huhitajika wakati wa usiku tu. Hata hivyo ikumbukwe kuwa joto katika nyumba ya vifaranga hubadilika kutegemeana na maeneo na majira tofauti ya mwaka.
Kama hali ya baridi ikizidi, muda wa kuwasha taa urefushwe, wakati wa joto taa zinaweza kuzimia mapema. Jambo la msingi ni mfugaji kuwa macho na kuwapa vifaranga joto la kutosha mara tu hali ya hewa ikibadilika. - CHAKULA NA MAJI. Ili vifaranga wakue vizuri wanahitaji chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika ambavyo ni protini, madini, wanga na vitamini pamoja na maji safi wakati wote. Hakikisha kuwa vyombo vya maji ni safi wakati wote.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.
Monday, November 21, 2016
NAMNA YA KUTENGENEZA JAM KWA KUTUMIA PASSION FRUIT.
Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye matandao(blog) wetu wa zinduka sasa tujifunze kuhusu namna ya kutengeza JAM kwa kutumia Passion fruit:
Vifaa:
Namna ya kuifadhi kwenye chupa:
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza namna ya kutengeza JAM kwa kutumia Passion fruit:
Vifaa:
- Matunda 36 toa kile kiini cha ndani (mbegu/juice) pamoja weka kwenye bakuli.
- Maganda ya Mapassion 12 ambayo umetoa mbegu na juice.
- Maji nusu kikombe yaliyotokana na maganda ya Passion.
- Nusu kikombe ya juice ya limao.
- Sukari: Kiasi cha sukari utayoweka itatokana na ni vikombe vingapi umepata kwenye mchanganyiko wa mbegu/juice na mchanganyiko wa maganda.
- Kata matunda yako 36 ya Passion na toa mbegu na Juice yake weka kwenye bakuli weka pembeni.
- Chukua maganda ya Mapassion 12 yale uliyotoa mbegu sawa na vipande 24 kwa sababu umevikata nusu.
- Weka kwenye sururia kubwa kiasi ya kuvitosha na weka maji yazidi nusu ya ile sufuria.
- Bandika jikoni na funika ile sufuria akikisha mfuniko ni wa hiyo sufuria ili ifunike vizuri mvuke ubakie ndani wakati inachemka.
- Chemsha kama lisaa limoja mpaka yale maganda yaive kabisa. Wakati yanachemka akikisha unayachanganya yale ya juu yanakwenda chini ili yaive na kulainika.
- Yakisha iva epua na yaache yapoe.
- Kama unayo fridge yaweke kwenye mpaka yawe ya baridi yalale kwenye fridge mpaka asubuhi.
- Maji uliyochemshia yatoe, lakini kumbuka kutoa nusu kikombe cha hayo maji ya maganda uliyochemsha.
- Chukua kijiko na chukua ganda moja moja toa kile kiini cha ndani ambacho kimeiva, kilaini na weka kwenye bakuli mpaka umalize kutoa maganda piece 24 ambayo ni maganda ya matunda 12.
- Ukishayaweka kwenye bakuli unaweza kuyapondaponda kiasi ili yalainike na ile ngozi ya ganda ya nje tupa. Kwani unachotaka hapo ni ile nyama ya Ganda ya ndani basi.
- Ukishapondaponda chukua ule mchanganyiko wa mbegu na juice yake na juice ya limao nusu kikombe changanya pamoja na maji nusu kikombe uliyotoa wakati umeshachemsha. Sasa changanya vitu vyote pamoja na pima huo mchanganyiko kwa vikombe viko vingapi.
- Kama ni vikombe vitano weka sukari vikombe vitano.
- Wakati umeweka kwenye sufuria ya kutosha tayari kuweka jikoni.
- Unaweza kutumia sufuria ukiyochemshia maganda.
- Sasa wakati ukiweka jikoni na ukaweka sukari punguza moto kiasi uku unakoroga mchanganyiko wa sukari na hivyo vitu vingine mpaka sukari inayeyuka.
- Sasa sukari ikishayeyuka unaongeza moto iendelee kuchemka na uku unakoroga Kama dk 35 hivi.
- Sasa ukitaka kujua Jam yako iko tayari chukua kisahani na chota ile Jam size ya kijiko cha chai.
- Akikisha wakati unapika unakorogea mwiko wa mbao siku zote usitumie mwiko wa Chuma ukiwa unapika Jam yeyote ni mbao au Plastic basi.
- Sasa chota kile kiasi weka kwenye kisahani acha kama dk moja hivi, na baada ya dk moja kuwa kama unamwaga au tumia kidole chako Kama unasukuma au kutoboa na utaona inaganda ata ukifanya Kama unamwaga inajishika kwenye kisahani. Lakini Kama iko maji maji sio kuganda/kunata endelea kuchemsha kwa dk nyingine chache na utaona inastic kwenye sahani .
- Epua na tayari unayo Jam ya kutumia.
Namna ya kuifadhi kwenye chupa:
- Wakati Jam ikishaiva unakuwa tayari umeshatayarisha chupa zako ambazo unachemsha maji unadumbukiza zile chupa kwenye yale maji ya moto.
- Mifuniko yake huwa inadumbukizwa kwenye maji ya uvuguvugu.
- Unaandaa sehemu safi kabisa maana hapa ndiko kwenye umakini kwenye kupaki Jam.
- Mara nyingi unatakiwa taulo safi kabisa umeweka juu ya meza. Jam ikiwa ndio iko jikoni umezima na tayari chupa ziko kwenye maji ya moto na mikono yako ni misafi kabisa kila chombo unachotumia lazima kipitie kwenye maji ya moto.
- Unatoa chupa kwenye maji na unachota jam na kuweka kwenye Chupa na unachukua kile kifuniko cha chupa na kufunika ile chupa kama nusu na unafanya hivyo kwa idadi ya chupa kulingana na size uliyotengeneza ya jam na wakati huo unakuwa na sufuria lingine linakuwa na maji tayari ya kuweka kuchemsha kwa dk 19.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza namna ya kutengeza JAM kwa kutumia Passion fruit:
Friday, November 18, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)