Tuesday, November 22, 2016

MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye matandao(blog) wetu wa zinduka sasa tujifunze kuhusu 

MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKKMK5WQyUtd39LB83gdLgj9sAMBP1fMppsb-JsytYG8xK9ML8Syf9DFlz0sIkmgTf2cL7OafRgSijXzqiItopIpP5oN-cels2KKMCydng45o-wEmGxO3hYGcTKNFY_hZRlfG9LQWysIw/s640/150304100318_chick_sexing_gch_pair_640x360_afp_nocredit.jpg

  1. KUWAPA JOTO. Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia kitalu ( mduara) unaoweza kutengenezwa kwa kutumia mbao na karatasi ngumu na kuweka chanzo cha joto ndani.
  2. UTOSHELEVU WA JOTO. Ufahamu utoshelevu wa joto kwa kuangalia tabia ya vifaranga wanapokuwa ndani ya Kitalu.

    Mfugaji unatakiwa kufuatilia vifaranga kwa karibu ili kutambua kama hali ya joto iliyopo inawafaa au laaah. Ufuatiliaji wa karibu husaidia kuchukua hatua mapema kama marekebisho yatahitajika.

    Kutegemeana na jinsi utakavyowaona vifaranga, fanya marekebisho mapema kabla madhara hayajatokea kwa vifaranga wako.

    Katika majuma 4 au 5 ya kwanza vifaranga huhitaji joto usiku na mchana na katika majuma 3 yanayofuata joto huhitajika wakati wa usiku tu. Hata hivyo ikumbukwe kuwa joto katika nyumba ya vifaranga hubadilika kutegemeana na maeneo na majira tofauti ya mwaka.

    Kama hali ya baridi ikizidi, muda wa kuwasha taa urefushwe, wakati wa joto taa zinaweza kuzimia mapema. Jambo la msingi ni mfugaji kuwa macho na kuwapa vifaranga joto la kutosha mara tu hali ya hewa ikibadilika.
  3. CHAKULA NA MAJI. Ili vifaranga wakue vizuri wanahitaji chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika ambavyo ni protini, madini, wanga na vitamini pamoja na maji safi wakati wote. Hakikisha kuwa vyombo vya maji ni safi wakati wote.

 

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza MATUNZO BAADA YA KUPOKEA VIFARANGA.

No comments:

Post a Comment