Monday, November 21, 2016

NAMNA YA KUTENGENEZA JAM KWA KUTUMIA PASSION FRUIT.

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye matandao(blog) wetu wa zinduka sasa tujifunze kuhusu namna ya kutengeza JAM kwa kutumia Passion fruit:
image

Vifaa:
  1. Matunda 36 toa kile kiini cha ndani (mbegu/juice) pamoja weka kwenye bakuli.
  2. Maganda ya Mapassion 12 ambayo umetoa mbegu na juice.
  3. Maji nusu kikombe yaliyotokana na maganda ya Passion.
  4. Nusu kikombe ya juice ya limao.
  5. Sukari: Kiasi cha sukari utayoweka itatokana na ni vikombe vingapi umepata kwenye mchanganyiko wa mbegu/juice na mchanganyiko wa maganda.
Namna ya kutengeneza:-
  1. Kata matunda yako 36 ya Passion na toa mbegu na Juice yake weka kwenye bakuli weka pembeni.
  2. Chukua maganda ya Mapassion 12 yale uliyotoa mbegu sawa na vipande 24 kwa sababu umevikata nusu.
  3. Weka kwenye sururia kubwa kiasi ya kuvitosha na weka maji yazidi nusu ya ile sufuria.
  4. Bandika jikoni na funika ile sufuria akikisha mfuniko ni wa hiyo sufuria ili ifunike vizuri mvuke ubakie ndani wakati inachemka.
  5. Chemsha kama lisaa limoja mpaka yale maganda yaive kabisa. Wakati yanachemka akikisha unayachanganya yale ya juu yanakwenda chini ili yaive na kulainika.
  6. Yakisha iva epua na yaache yapoe.
  7. Kama unayo fridge yaweke kwenye mpaka yawe ya baridi yalale kwenye fridge mpaka asubuhi.
  8. Maji uliyochemshia yatoe, lakini kumbuka kutoa nusu kikombe cha hayo maji ya maganda uliyochemsha.
  9. Chukua kijiko na chukua ganda moja moja toa kile kiini cha ndani ambacho kimeiva, kilaini na weka kwenye bakuli mpaka umalize kutoa maganda piece 24 ambayo ni maganda ya matunda 12.
  10. Ukishayaweka kwenye bakuli unaweza kuyapondaponda kiasi ili yalainike na ile ngozi ya ganda ya nje tupa. Kwani unachotaka hapo ni ile nyama ya Ganda ya ndani basi.
  11. Ukishapondaponda chukua ule mchanganyiko wa mbegu na juice yake na juice ya limao nusu kikombe changanya pamoja na maji nusu kikombe uliyotoa wakati umeshachemsha. Sasa changanya vitu vyote pamoja na pima huo mchanganyiko kwa vikombe viko vingapi.
  12. Kama ni vikombe vitano weka sukari vikombe vitano.
  13. Wakati umeweka kwenye sufuria ya kutosha tayari kuweka jikoni.
  14. Unaweza kutumia sufuria ukiyochemshia maganda.
  15. Sasa wakati ukiweka jikoni na ukaweka sukari punguza moto kiasi uku unakoroga mchanganyiko wa sukari na hivyo vitu vingine mpaka sukari inayeyuka.
  16. Sasa sukari ikishayeyuka unaongeza moto iendelee kuchemka na uku unakoroga Kama dk 35 hivi.
  17. Sasa ukitaka kujua Jam yako iko tayari chukua kisahani na chota ile Jam size ya kijiko cha chai.
  18. Akikisha wakati unapika unakorogea mwiko wa mbao siku zote usitumie mwiko wa Chuma ukiwa unapika Jam yeyote ni mbao au Plastic basi.
  19. Sasa chota kile kiasi weka kwenye kisahani acha kama dk moja hivi, na baada ya dk moja kuwa kama unamwaga au tumia kidole chako Kama unasukuma au kutoboa na utaona inaganda ata ukifanya Kama unamwaga inajishika kwenye kisahani. Lakini Kama iko maji maji sio kuganda/kunata endelea kuchemsha kwa dk nyingine chache na utaona inastic kwenye sahani .
  20. Epua na tayari unayo Jam ya kutumia.
Hiyo ni ya kutumia nyumbani kwako na unaweza kukaa nayo mpaka miezi sita kama umetengezeza nyingi.

Namna ya kuifadhi kwenye chupa:
  1. Wakati Jam ikishaiva unakuwa tayari umeshatayarisha chupa zako ambazo unachemsha maji unadumbukiza zile chupa kwenye yale maji ya moto.
  2. Mifuniko yake huwa inadumbukizwa kwenye maji ya uvuguvugu.
  3. Unaandaa sehemu safi kabisa maana hapa ndiko kwenye umakini kwenye kupaki Jam.
  4. Mara nyingi unatakiwa taulo safi kabisa umeweka juu ya meza. Jam ikiwa ndio iko jikoni umezima na tayari chupa ziko kwenye maji ya moto na mikono yako ni misafi kabisa kila chombo unachotumia lazima kipitie kwenye maji ya moto.
  5. Unatoa chupa kwenye maji na unachota jam na kuweka kwenye Chupa na unachukua kile kifuniko cha chupa na kufunika ile chupa kama nusu na unafanya hivyo kwa idadi ya chupa kulingana na size uliyotengeneza ya jam na wakati huo unakuwa na sufuria lingine linakuwa na maji tayari ya kuweka kuchemsha kwa dk 19.
N.B: Unaweza kuchanganya matunda zaidi ya moja, mfano Passio na mango au Papaya au Apple na unaweza kuweka viungo kwa mbali kama ginger au mdalasini kuleta harufu ya hicho kiungo.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza namna ya kutengeza JAM kwa kutumia Passion fruit:




No comments:

Post a Comment