Thursday, November 17, 2016

UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI

 UTAMBUZI WA MAGONJWA YA KUKU KUPITIA RANGI YA KINYESI
Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye matandao(blog) wetu wa zinduka sasa tujifunze namna ya kutambua magonjwa ya kuku kupitia rangi ya kinyesi.
  1. Mharo mweupe(pullorum bacilary diarrhoea) ugonjwa huu huathiri zaidi vifaranga kabla ya wiki nne huharisha mharo mweupe.
    TIBA
    kuu ni usafi pekee kwenye banda na kuepusha maji yasimwagike ovyo.
     
  2. KIPINDUPINDU CHA KUKU(fowl cholera) kinyesi cha kuku ni njano.
    TIBA: Tumia dawa za salfa, eg Esb3 au amprollium.
     
  3.  COCCIDIOSIS mwanzo kinyesi cha kijivu na baadae huharisha damu iliyochanganyika
    TIBA: Tumia dawa ya VITACOX au ANTICOX
     
  4. MDONDO(Newcastle) kuku hunya kinyesi cha kijani sio kila kijani ni newcastle
    TIBA: HAKUNA TIBA
    . Ila tumia vitamini na antibiotic
  5. TYPHOID Kinyesi cheupe kinagandia sehemu za nyuma au hulowana sehemu za haja.
    TIBA: Dawa ni Eb3
     
  6. GUMBORO Huathiri zaidi vifaranga kinyesi huwa ni majimaji
    TIBA: HAKUNA DAWA.
    Ila tumia vitamini na antibiotic   
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi juu ya namna unavyoweza kupata utambuzi wa magonjwa ya kuku kupitia rangi ya kinyesi. 

No comments:

Post a Comment