Tuesday, November 1, 2016

JINSI USINGIZI UNAVYOWEZA KULETA MATATIZO YA UZAZI

Hujambo rafiki karibu sana kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze jinsi usingizi unavyoleta matatizo ya uzazi.
Image result for how to sleep
Utafiti uliofanywa umeonyesha kuwa wanaume wengi wako kwenye hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya uzazi kutoka na kulala sana au kulala chini ya kiwango kinachotakiwa.

Kwa kiwango kinachotakiwa, mtu hutakiwa kulala kati ya saa saba hadi nane kwa siku.
Uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu ch Boston nchini Marekani kwa kutumia sampuli ya watu 790 ilionyesha kuwa kulala chini ya saa sita au zaidi ya saa tisa kwa siku husababisha mwanaume kupata matatizo ya uzazi ikiwa ni pamoja na kupungua kwa nguvu za kiume.
Kwa wanaume hao waliofanyiwa utafiti ambapo baadhi walilala chini ya saa sita na wengine zaidi ya saa tisa, walikuwa na hatari ya kushindwa kuwapa ujauzito wake zao kwa asilimia 42.

Sababu kubwa ni kuwa kulala bila kuzingatia muda unaotakiwa kunasababisha kuathiriwa kwa vichocheo vya mwili. Vichocheo hivyo vya mwili viitwavyo testosterone huzalishwa katika mwili wa mwanaume wakati amelala, walieleza wataalamu hao. Hivyo wakahitimisha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya muda unaotumiwa na mwanaume kulala na uzalishaji wa vichocheo kwa ajili ya nguvu za kiume.

Mbali na kuwa kulala kwa muda mfupi kuna athiri nguvu za kiume, lakini pia kuna madhara mengine kiafya ikiwa ni pamoja na huathiri afya ya akili na pia uwezo wa mtu kufanya kazi sababu anakuwa na uchovu kwa kutokupata muda wa kutosha kupumzika.
Msongo wa mawazo pia huathiri ukuaji wa binadamu hata afya yake ya akili.

Asante sana kwa kitutembelea na kujifunza vya kutosha.






No comments:

Post a Comment