Wednesday, October 12, 2016

KUTENGENEZA MANGO PICKLE (achali ya EMBE)YAKUPIKWA NA ISIYOPIKWA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze namna ya kutengeneza mango pickle (achali ya embe)MANGO  PICKLES au  "ACHARI  YA  EMBE"  ni  chachandu  inayo  tumika  kunogesha  utamu  wa  chakula.   Malighafi  kuu  katika  utengenezaji  wa  "MANGO  PICKLES "  ni  embe

Maitaji

  1. Nunua embe mbichi kabisa
  2. Chumvi
  3. Pilipili ya unga
  4. Nyanya
  5. Vitunguu na karot
  6. Pilipili mtama na iriki kama ukipenda inukie
  7. kitunguu saum

KUTENGENEZA

  1. Bandika sufuria yako jikoni iwe kwenye moto weka mafuta ya kula kaanga vitunguu
  2. Kisha kitunguu saum, weka karot, hoho kaanga
  3. Kisha nyanya wakati huo ulishaandaa maembe kwa kuyakata vipande upendavyo ila vidogo vinapendeza  changanya na pilipili ya unga na chumvi vijiko viwili changanya peke ake pembeni weka chuja maji mana huwa vinatoaga maji hakikisha vimechanganyika vizuri na pilipili.
  4. Kisha vitose kwenye lost yako mpaka viive tayari kwa kuuzwa vipaki kwenye vikopo.

Hapa tunatengeza kwa ajili ya biashara na huwa inakaa miezi 3 hadi 6

ISIYOPIKWA

Mahitaji:

  1. embe
  2. vinager
  3. mafuta ya alizeti aldari
  4. uwatu
  5. pilipili masala
  6. vifungashio Lebo na sili.

KUANDAA
Jinsi ya kuandaa sasa ili iende sokon.

  1. Embe mbichi kabisa iwe dodo au tanga osha embe na katakata vipande vidogo saizi ya wastani hakikisha umeoshaa na maji safi na salama.
  2. Chukua ndoo weka vipande vya embe changanya na chunvi funika acha siku 5/21
  3. Baada ya hapo utachukua embe zako na kuziosha tena ili kupunguza chumvi.
  4. Baada ya hapo changanya kwa pamoja kisha jaza kwenye chupa sindilia vema ktk chupa ili kusiingie hewa na pia wakati unandaa zingatia usafi wa mikono na vitendea kazi hili la muhimu sana
  5. ukumaliza chukua mafuta ya alizeti pasha moto kisha utakuwa unaweka vijiko 2 pale juu ya mango pickle yako usijaze chupa ili kulinda bidhaa yako isiharibiki ukimaliza chukua chupa zako weka lebo na sili. Hapo zinakuwa Hapo zinakuwa tayari peleka sokoni

NB: Hii haipikwi tuelewane

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu achali ya embe.

 

MAVUNO NA MAPATO YATOKANAYO NA ZAO LA SOYA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo katika sehemu ya mwisho wa zapo la SOYA tujifunze MAVUNO NA MAPATO YATOKANAYO NA ZAO LA SOYA

Mavuno
Soya ina uwezo wa kutoa kilo 1,500 hadi 2,500 kwa hekta kutegemea na aina, hali ya hewa, rutuba ya udongo, matumizi ya mbolea na utunzaji kuanzia wakati wa kuchagua mbegu, kulima, kupanda na kuvuna. Kiasi hicho cha mavuno ni sawa na kilo 600 hadi 1,000 kwa ekari moja.
Mapato Kutokana na mavuno ya soya, mkulima anaweza kupata mapato mengi ukilinganisha na mazao kama mahindi na maharage kwa eneo lililosawa na eneo la soya.
Ukweli huu unabainishwa na tathmini iliyofanyika mwaka wa 2005 na Wizara ya Kilimo na Chakula, juu ya hali kilimo cha soya nchini. Tathmini hiyo ilionyesha kuwa wastani wa gharama za kuzalisha kilo moja ya soya kwa mikoa ya Nyanda za Juu za Kusini hususan Songea Vijijini ni shilingi 130, kwa hiyo kama mkulima atauza soya kwa wastani wa shilingi mia mbili (200) kwa kilo moja bila gharama ya kusafi risha mbali na kijijini kwake anaweza kupata faida ya kati ya shilingi 105,000 hadi 175,000 kwa hekta moja au kati ya shilingi 42,000 na 70,000 kwa ekari moja.
Hata hivyo mapato yanaweza kuongezeka endapo mkulima atatunza na kuuza soya wakati bei imepanda kwa kuwa soya inaweza kutunzwa muda mrefu bila kuharibiwa na wadudu. Ni dhahiri kuwa zao la soya linaweza kumuongezea mkulima kipato na kumuondolea umaskini.
Screenshot-8.png
Screenshot-9.png

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu zao la SOYA kuanzia siku ya kwanza mpaka leo usikose mfululizi wa mafunzo mengi yatakayofuata kupitia mtandao huu.

Monday, October 10, 2016

KUVUNA, KUPURA NA KUHIFADHI SOYA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo katika tujifunze jinsi ya KUVUNA, KUPURA NA KUHIFADHI SOYA.

 
Kuvuna Soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji wa shamba. Kwa mfano soya aina ya Bossier huchukua miezi mitatu hadi minne kukomaa na aina ya Uyole Soya 1 miezi minne hadi mitano. Dalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya njano.

Anza kuvuna baada ya majani kuanza kupukutika. Soya ikikauka, maganda yake hupasuka na mbegu hupukutikia chini. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi kuvuna soya mara inapokomaa na kuanza kukauka. Ili kuzuia upotevu wa zao shambani, inashauriwa kuvuna majira ya asubuhi au majira ambayo sio ya jua kali endapo soya imekauka na kuanza kupasuka wakati wa kuvuna. Kupura Soya haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu zake hupasuka kirahisi. Mara baada ya kupura, ondoa takataka na uchafu mwingine kwenye soya kwa kupepeta na kupembua. Kausha soya kufi kia wastani wa asilimia 10 ya kiasi cha maji (moisture moisture content content) kisha ihifadhi ghalani kwa matumizi au kusubiri soko.
Screenshot-6.png
Screenshot-7.png
Kuhifadhi
Hifadhi soya baada ya kuhakikisha kuwa imekauka vizuri. Ni muhimu kuhifadhi soya mahali pakavu ili soya isipate uvundo na kuharibu soya ya mbegu na ya chakula. Soya inaweza kuhifadhiwa kwenye vihenge au kwenye magunia kama mazao mengine, tofauti ni kutohitajika dawa ya kuhifadhia.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi usikose sehemu itakayofuata ya somo hili.

 

UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA
Screenshot
Kutayarisha shambaShamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage). Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha sesa kinaweza kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha matuta kukinga mteremko kinafaa na kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko. Vilevile kilimo cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.
Screenshot-
MbeguNi muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa mtaalam aliyekaribu naye kabla ya kuamua kulima soya.
Aidha, mkulima anashauriwa kununua na kutumia mbegu kutoka katika sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano wa sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala wa mbegu, mashamba ya mbegu na vituo vya utafiti. Hii ni kwa sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji katika msimu mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota.
Kama mkulima hana uhakika na chanzo cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo ya uotaji (germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni kuzilowesha mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali penye joto la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka zitakapoota. Hesabu mbegu zilizoota na iwapo mbegu zilizoota ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani asilimia 75, mkulima anashauriwa kutopanda mbegu hizo.
Wakati wa kupandaUpandaji wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa aina za soya zinazokomaa mapema, soya ikipandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa kipindi kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha na hivyo kufanya uvunaji na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu zitaoza au kuanza kuota na kupoteza ubora wake.
Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya kulingana na mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa soya inakomaa wakati hakuna mvua ili kurahisisha uvunaji na soya kutooza.
Jedwali linaonyesha mahali, aina na muda wa kupanda soya.
  Screenshot0
Nafasi ya kupandaMkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo ni sentimeta 10 kwa sentimita 45 kwa soya fupi kama bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafi fu. Aidha, tumia sentimeta 10 kwa sentimita 60 kwa soya ndefu kama Uyole Soya 1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi. Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita tano ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya. Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya kabla ya kupanda.

PaliziSoya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza isihitajike ambapo soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa imekua na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya pili kutohitajika. Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa kufuata
WADUDU, MAGONJWA NA WANYAMA WAHARIBIFU
Wadudu

Kwa sasa, nchini Tanzania soya haishambuliwi sana na wadudu kama ilivyo sehemu nyingine ambako zao hilo hulimwa kwa wingi. Hata hivyo endapo wadudu watatokea mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50% EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao.
Tofauti na mazao kama mahindi na maharage, hakuna wadudu waharibifu wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza kutunzwa kwa muda mrefu ghalani bila kuwa na athari za wadudu. Kwa mkulima na wafanyabiashara, kutokuwepo wadudu waharibifu ghalani kunapunguza gharama za utunzaji hadi bei nzuri itakapofi kiwa.
Magonjwa
Kama ilivyo kwa wadudu, magonjwa ya soya ni machache. Hata hivyo magonjwa ambayo hutokea kwa nadra ni yale yanayotokana na vimelea vya ukungu na bakteria. Magonjwa hayo huenezwa kwa mbegu, masalia ya mimea shambani na wadudu mafuta. Hivyo ni bora kwa mkulima kuzingatia kanuni za kilimo bora au kupata ushauri wa kitaalamu ili kuepukana na magonjwa hayo. Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa katika zao la soya ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali husika.
Aidha, panda kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia mazao yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya kama alizeti na mahindi. Wanyama waharibifu Kwa kawaida soya hupendwa sana na panya wa shambani na ghalani. Wanyama wengine ni pamoja na sungura, paa, swala, n.k. Mkulima anashauriwa kutumia mbinu na njia mbalimbali zikiwemo za asili, kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu mazingira.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi usikose sehemu itakayofuata ya somo hili.

Saturday, October 8, 2016

ZIFUATAZO NI FURSA AMBAZO ZINAWEZA KUKUTOA KIMAISHA

Hajambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze FURSA AMBAZO ZINAWEZA KUKUTOA KIMAISHA. Watu wengi wamekuwa wakiangaika ama kuwauliza watu wao wa karibu ni biashara gani afanye au ukimuuliza ni biashara gani unataka kufanya atakuambia mimi nataka kufanya biashara yoyote ili mradi tu iwe inaniingizia faidi.
Kuwa specific na usipende kufanya biashara yoyote kwani kama ujui unataka kwenda wapi basi uelekeo wowote utakupeleka usipotaka. Si mawazo yote yatakuwa sawa kwako,chagua wazo moja tu la biashara  na uanze kulifanyia kazi na uanze sasa kwa kutumia chochote ulichonachoo usingoje kuwa na fedha nyingi ndiyo uanze.
Chagua eneo gani upo vizuri na kuchukua hatua sasa.

ZIFUATAZO NI FURSA AMBAZO ZINAWEZA KUKUTOA KIMAISHA 
  1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. 
  2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. 
  3. Kutengeneza na kuuza tofali. 
  4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali. 
  5. Kuanzisha kituo cha redio na televisheni. 
  6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano. 
  7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k 
  8. Kushona na kuuza nguo. 
  9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali. 
  10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine. 
  11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo. 
  12. Kutoa ushauri mbalimbali waKitaalamu. 
  13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza. 
  14. Kusajili namba za simu na kuuzavocha.
  15. Kuwa na mradi wa Pikipiki. 
  16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika. 
  17. Kuuza Mitumba. 
  18. Kusimamia miradi mbalimbali 
  19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali. 
  20. Kufungua banda la chakula na chips. 
  21. Kukodisha turubai viti na meza. 
  22. Kufungua Supermarket. 
  23. Kufungua Saluni. 
  24. Kufungua Bucha. 
  25. Video Shooting & Editing. 
  26. Kufungua Internet cafe. 
  27. Duka la kuuza matunda. 
  28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline. 
  29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati. 
  30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT. 
  31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k 
  32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor). 
  33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k. 
  34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja. 
  35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora. 
  36. Kukodisha Music 
  37. Kuanzisha Mradi wa Taxi 
  38. Kuanzisha mradi wa Daladala. 
  39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine. 
  40. Kununua magenerator na kukodisha 
  41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu. 
  42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP). 
  43. Kuuza mabati na vigae 
  44. Kujenga apartments 
  45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote. 
  46. Kufungua Duka la samaki. 
  47. Kufungua Duka la nafaka. 
  48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo. 
  49. Kujenga hostel 
  50. Kuuza vocha na vingamuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG,Digitech, Continental. 
  51. Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi. 
  52. Ufundi simu 
  53. Kufungua Hospitali, Zahanati. 
  54. Maabara ya Macho, Meno 
  55. Kuchimba/Kuuza Madini 
  56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax. 
  57. Kuuza miti na mbao. 
  58. Kufungua Grocery, bar 
  59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha. 
  60. Kucharge simu/battery. 
  61. Duka la TV na vifaa vingine. 
  62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering). 
  63. Banda la kupigisha simu. 
  64. Kuuza na kushona Uniform za shule. 
  65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla. 
  66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari 
  67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe 
  68. Kuuza fanicha. 
  69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na mitambo. 
  70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel) 
  71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium. 
  72. Kuuza vioo 
  73. Kushona na kukodisha nguo za harusi. 
  74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari 
  75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine). 
  76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc) 
  77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi 
  78. Kufungua studio ya kutengenezavipindi vya redio na televisheni 
  79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games) 
  80. Kufungua benki. 
  81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga. 
  82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k 
  83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali. 
  84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane) 
  85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu. 
  86. Kuanzisha viwanda mbalimbali 
  87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k 
  88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali 
  89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha 
  90. Kutengeneza antenna na kuuza 
  91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao 
  92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo 
  93. Biashara ya kuagiza magari 
  94. Kufanya biashara za Jukebox 
  95. Kukodisha matenki ya maji 
  96. Kufungua duka la kuuza Asali 
  97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha 
  98. Kufungua Duka la vinyago, batiki 
  99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZYPESA  
  100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym). 
  101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi. 
  102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy). 
  103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi 
  104. Kufungua kampuni ya"Clearing and fowarding" 
  105. Kuchezesha vikaragosi 
  106. Kuuza spea za bajaji, magari napikipiki 
  107. Kuuza baiskeli 
  108. Kuuza magodoro 
  109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe,vijiko
  110.  Kuuza marumaru (limestones) 
  111. Kuuza kokoto 
  112. Kuuza mchanga 
  113. Kufundisha Tuisheni 
  114. Biashara za bima 
  115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege) 
  116. Biashara za kitalii 
  117. Biashara za meli na maboti. 
  118. Kampuni ya kuchimba visima 
  119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea 
  120. Kuuza mkaa 
  121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofal 
  122. Kampuni ya kupima ardhi 
  123. Kampuni ya magazeti 
  124. Kuchapa (printing) magazeti 
  125. Kuuza magazeti 
  126. Kuchimba mafuta 
  127. Kiwanda cha kutengeneza mabati 
  128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha 
  129. Kiwanda cha kutengeneza matairi 
  130. Kutengeneza vitanda vya chuma 
  131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha. 
  132. Kukodisha makapeti 
  133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe. 
  134. Mashine ya kusaga na kukoboanafaka. 
  135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha. 
  136. Kuuza Gypsum 
  137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo 
  138. Duka la kuuza mboga za majani 
  139. Duka la kuuza maua. 
  140. Kampuni ya kuzoa takataka 
  141. Kampuni ya kuuza magari 
  142. Kuuza viwanja 
  143. Uvuvi 
  144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi 
  145. Uchoraji wa mabango 
  146. Duka la kuuza silaha 
  147. Ukumbi wa kuonesha mpira 
  148. Biashara ya Multi-Level Marketing-MLM 
  149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari 
  150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo...
Amua haraka nini unataka kufanya kwa ajili yako na maisha yako na kama kweli unataka kufanya biashara/ujasiriamali  napenda kukusisitiza uanze sasa.Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza FURSA AMBAZO ZINAWEZA KUKUTOA KIMAISHA.

Wednesday, October 5, 2016

UJUE MMEA WA MLONGE

Haujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze faida na umuhimu wa mmea wa mlonge.
images


Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.
Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mjibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka shilingi 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walipokuwepo hapa Tanzania bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu.
Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.
MLONGE UNA:
Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt) Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach Una vitaminis Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla
MLONGE NDICHO CHAKULA CHENYE AFYA ZAIDI KULIKO CHAKULA KINGINE CHOCHOTE JUU YA ARDHI;
Mlonge una jumla ya virutubishi 92. Mlonge unaondoa sumu na huondoa uvimbe mbalimbali mwilini, una asidi amino 18 na asidi amino mhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.
Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini, magonjwa hayo ni pamoja na;
1. Huko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu Kisukari
2. Huko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
3. Hutibu matatizo au maumivu ya mishipa
4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo (stroke),
5. Hutibu Kansa
6. Pumu
7. Hutuliza wasiwasi
8. Kikohozi
9. Maumivu ya kichwa
10. Inazuia na kushusha lehemu (cholesterol) hata ile ya juu zaidi (hypocholesteremia)
11. Inapunguza mafuta tumboni
12. Inaweka sawa homoni
13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi (dysmenorrhea),
14. Unasafisha ini (hepatic detoxification),
15. Unasafisha mkojo na kibofu cha mkojo
16. Unarekebisha matatizo kwenye tezi
17. Unatibu kipindupindu na kuharisha
18. Kifua kikuu
19. Kichwa kizito
20. Uchovu
21. Mzio (aleji)
22. Vidonda vya tumbo
23. Maambukizi kwenye ngozi
24. Maumivu mbalimbali mwilini
25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi (blackheads),
26. Husafisha damu,
27. Hutibu matatizo kwenye koo
28. Huondoa makohozi mazito kooni
29. Huondoa taka na msongamano kifuani
30. Hutibu kipindupindu
31. Huondoa mtoto wa jicho au uvimbe kwenye jicho
32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio
33. Unatibu homa
34. Maumivu kwenye maungio
35. Huondoa chunusi
36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili
37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji
38. Inatibu Kiseyeye (scurvy)
39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla
40. Unatibu minyoo
41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha
42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana (colitis)
43. Unatibu gauti (dropsy),
44. Unatibu kuhara damu (dysentery)
45. Unatibu kisonono ( gonorrhoea)
46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi,
47. Unatibu homa ya manjano (jaundice),
48. Unatibu malaria
49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo
50. Unasidia pia kujenga na kuimarisha misuli
51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge unasafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno, ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya (fresh) na mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.
Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas (aina ya nishati ya umeme inayotokana na kinyesi cha ng’ombe au takataka). Hutumika pia kama chakula cha wanyama kama sungura, mbuzi, ng’ombe, mbwa nk. Sungura wanaonekana kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.
MBEGU ZA MLONGE:
molinga-seed 

1. Mbegu zake hutumika kama kiuaji sumu na pia hutibu uvimbe. Hutibu maumivu ya kwenye mishipa, baridi yabisi, gauti, kukamaa mishipa, magonjwa ya ngono na majipu. Mbegu hizi hukaangwa kidogo, hupondwapondwa na kuchanganywa na mafuta ya nazi na kupakwa sehemu yenye tatizo.
2. Mbegu za mlonge zilizokaangwa na mafuta yake husaidia watu wanaoshindwa kuzalisha mkojo.
3. Mbegu zake hutumika pia kumtuliza au kumfanya mtu mwenye kifafa a-‘relax’.
4. Mbegu za mti wa Mlonge ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi ikiwemo fangasi.
5. Pia mbegu hutumika katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa badala ya kuchemsha.
6. Mbegu za mlonge pia huongeza kwa kiasi kingi kinga ya mwili (CD4), Kama una tatizo la kinga ya mwili wako kushuka basi tumia mbegu za mlonge kwa mwezi mmoja mpaka mitatu na kinga yako itaimarika sana.
Chukuwa punje 3 na uzimenye ganda lake la juu na utafune mbegu ile ya ndani yote hizo tatu na ukimaliza kuzitafuna kunywa maji ya kawaida siyo ya kwenye friji glasi 2 (nusu lita), fanya hivi kutwa mara tatu.
MLONGE UNATOA WAPI MAAJABU YOTE HAYA?
Matatizo mengi ya kiafya ni matokeo ya lishe yenye viinilishe duni au hafifu jambo linalopelekea kuwa na kinga ya mwili isiyo na nguvu kupigana na magonjwa mbalimbali. Unaporekebisha usawa huo usio sawa wa kinga yako ya mwili kwa kutumia mimea na lishe zingine mhimu za asili hutakawia kuona matokeo mazuri kwenye afya yako.

Uwezo wa mti wa mlonge kuyaweza yote hayo ni kutokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondowaji sumu vingi kuliko mmea mwingine wowote. Wagonjwa wengi wenye UKIMWI katika sehemu nyingi za Afrika magharibi wameripoti kuongezeka kiasi kikubwa cha kinga yao ya mwili baada ya kutumia mlonge kiasi cha kutokuhitaji dawa.
NGUVU, UMAKINI, NGOZI YENYE KUPENDEZA, KUTOZEEKA MAPEMA NA KUPUNGUZA UZITO NA UNENE:
Mlonge una viinilishe mhimu vinavyosaidia kuuongezea uwezo mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vitamini, madini na homoni mhimu zilizomo kwenye mti huu huufanya mwili wako kuwa na usawa unaohitajika kiafya na hivyo kukupa kinga dhidi ya magonjwa mengi bila idadi.

Mlonge una kiinilishe mhimu sana kwa wingi kuliko mmea au mti mwingine wowote duniani mara maelfu kadhaa kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘Zeatin’. Zeatin ndiyo hutengeneza seli mpya za ngozi pia huzifanya seli mpya kutengenezwa kwa haraka na kwa wingi zaidi ya zile seli zinazokufa. Hii huleta matokeo mazuri ikiwemo kuondoa mikunjo ya ngozi au ngozi kuzeeka sehemu za uso na sehemu nyingine za mwili na kukupa afya nzuri ya ngozi.
Kwenye mlonge kuna ‘Sulfur’, hii sulfur ni mhimu katika kuunda vitu mhimu kwenye ngozi kama collagen na keratin huku viuaji au viondowaji sumu zaidi ya 30 vinavyopatikana kwenye mlonge ni mhimu kwa ajili ya afya ya ngozi yako.
Mlonge ambao umekuwa ukitumika kwenye vituo vingi vinavyojihusisha na kupunguza uzito huwa una nguvu ya asili ya kupunguza njaa, huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kukung’arisha wewe huku ukikuacha na virutubishi vingi mhimu zaidi.
HUIRUDISHA UPYA AFYA YA MWILI WAKO;
Baada ya kufikisha umri wa miaka 30 hivi nguvu zako za mwili huanza kushuka. Mwili wako utaanza kuleta mchonyoto. Utaona unaanza kupoteza umakini nyakati za mchana sababu hukuzingatia nini ule wakati ulipokuwa kijana. Baadhi ya kuharibika kwa afya hakuwezi kurudishwa nyuma ikiwa ni pamoja na kuzorota kwa afya ya meno.

AFYA MBOVU YA MENO INAPELEKEA MAGONJWA KADHAA NA VIFO;
Calcium, Magnesium, Manganese, Potassium, Boron na Vitamini D yote ni madini mhimu ili uwe na meno yenye afya. Magonjwa mengi sugu ni matokeo ya upasuaji wa kwenye kinywa. Kila mtu anapaswa kulinda afya ya meno yake kuanzia leo kwani meno yakishaoza au kuharibika huwa ni vigumu kupona na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo. Afya ya meno yako itaamua ni miaka mingapi unaweza kuishi.

Kila mmoja wetu anatakiwa kutimiza wajibu wake linapokuja suala la afya ya mwili wako. Tumia google tafuta taarifa za kile unachokula au kunywa kila siku. Kichwa kitakuuma utakapojua ni nini unakula!. Nenda YouTube angalia video hizi: “Food Matters” na “Dying to have know”. Tafuta kwenye chaneli ya Discovery movie inaitwa “Moringa The Miracle Tree” na video nyingine inaitwa ‘Moringa Oleifera’.
BIDHAA NYINGI ZA AFYA HAZINA AFYA YOYOTE;Bidhaa nyingi za afya hazina utafiti halisi (genuine) unaojitegemea au zina maelezo kutoka kwa mtengenezaji tu wa hiyo bidhaa. Mlonge una mfululizo wa tafiti za watu wengi na shuhuda za watu kote duniani zaidi ya miaka 4000 iliyopita. Ni mtishamba kwa asilimia 100 unaoota wenyewe.
Matumizi ya mlonge kama kiua vijasumu (antibiotic) kwenye tiba asili yalianza miaka maelefu iliyopita. Mlonge ulitumika kwa mara ya kwanza kama dawa zaidi ya miaka 2000 kabla ya Kristo. Watabibu wazamani wa Misri na Ugiriki waliona faida nyingi za mti huu na wakautambulisha kwa Warumi na baadaye mlonge ukaenea mashariki mwa India na sehemu ya chini ya nchi ya Uchina, kusini mashariki mwa Asia na Ufilipino na magharibi mwa Misri kuzunguka mediterania na mwishowe ukafika kwa Wahindi mashariki mwa Amerika. Leo zaidi ya watu milioni 400 wanatumia mlonge. Shirika la afya duniani (W.H.O) limekuwa likitumia mlonge zaidi ya miaka 40 sasa.
Unga wa majani ya mlonge unapaswa uwe ni wa kijani kweli kweli na majani yake yawe yalianikwa kivulini na siyo juani. Anza na kijiko kidogo kimoja ukichanganya na vimiminika kama maji ya uvuguvugu au juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani kutwa mara moja na taratibu ongeza kiasi cha dawa kadri unavyohitaji. Unaweza kuuchanganya pia kwenye wali wakati unakula au unaweza kuweka ndani ya kikombe cha uji au unaweza kutumia kama majani yako ya chai ingawa hautakiwi uchemshe sana kwenye moto.
Mti wa mlonge sasa umeanza kuwa maarufu huko Marekani hii ni kutokana na mti wenyewe kuendelea kupata umaarufu miongoni mwa watu wanaojali afya zao. Ingia google andika ‘Moringa plants for sale’ utagundua keyword hiyo inatafutwa kila siku mara maelfu. Watu wengi pia wameanza kilimo cha mlonge kama biashara ya kuwaingizia kipato. Ukiwa na miti 200 tu ya mlonge shambani kwako tayari wewe siyo mwenzetu.
Mti wa mlonge ni moja ya miti mhimu katika sehemu yote ya dunia. Kadri watu wanavyoendelea kuutafiti na kuusoma mti huu ndivyo mahitaji ya unga wa majani yake, mbegu zake, unga wa mbegu zake na mafuta ya mbegu zake yatakavyozidi kuongezeka na kuongezeka.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu mmea wa mlonge mengi yatafuata endelea kutufuatilia.

Tuesday, October 4, 2016

HUYU NDIYE FULUGECIO BATISTA

 Haujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze historia fupi ya kiongozi wa zamani wa Cuba ambaye alitengeneza historia kubwa  na alileta changamoto nyingi sana katika nchi ya Cuba.

Fulgencio Batista Zaldivar (Januari 16, 1901 - 6 Agosti 1973) zaidi anajulikana kama Fulgencio Batista, alichaguliwa kuwa Raisi wa Cuba 1940-1944, na dikteta 1952-1959, kabla ya kuangushwa katika Mapinduzi ya Cuba
. Batista25355a crop4.jpg
Batista awali mwaka 1933 alikuwa sehemu ya maofisa wa mapinduzi na kupindua utawala wa kimabavu wa Gerardo Machado. Batista kisha alijiteua mwenyewe kama mkuu wa vikosi vya kijeshi. Aliweza kuongoza na kuwadhibiti marisi vibaraka mpaka 1940, na ndio wakati yeye mwenyewe alichaguliwa kuwa Rais wa Cuba. Kisha akasisitiza kuundwa kwa katiba ya 1940 kwa wanacuba na kutumikia Cuba hadi mwaka 1944. Baada ya kumaliza kipindi chake aliishi nchini Marekani, na alirudi tena Cuba kugombea urais mwaka 1952. Ilipelekea kushidwa sana katika uchaguzi ule ambapo alitumia jeshi ili kuingia madarakani.

Aliporudi madarakani kwa nguvu, Batista alisitisha katiba ya Cuba ya mwaka 1940 na kubadili mwelekeo wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuminya haki ya maandamano. Kisha alitengeneza urafiki na wamiliki wakubwa wa ardhi na mashamba ambao walikuwa ni wakulima wa miwa na hii ilipelekea mdororo wa kiuchumi kiasi ya kwamba kukawa na matabaka mawili ambayo ni matajiri na maskini. Serikali ya Batista ilizidi rushwa na kandamizi kiasi ya matajiri hawa kutengeneza faida kubwa kwa kuwanyonya maskini vile vile alitengeneza urafiki na wamafia wa kimarekani waliokuwa wanafanya biashara haramu kama ya madawa ya kulevia, ukahaba huko Havana.
Kuchochea upinzani dhidi ya mbinu hizo, kwa miaka miwili (Desemba 1956 - Desemba 1958) Julai 26 Fidel Castro na washirika wengine wazalendo walianzisha vita ya msituni dhidi ya serikali ya kidhalimu ya Batista, vita ambayo iliongozwa chini ya muasi machachari Che Guevara mwaka 1959. Batista na washirika wake mara moja walikimbilia visiwa vya Jamhuri ya Dominika. Batista hatimaye kupatiwa hifadhi ya kisiasa nchini Ureno, ambako aliishi mpaka kufa kwa ugonjwa wa moyo Agosti 6, 1973, karibu na Marbella, Ureno.

Asante sana kwa kutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu historia Batista usikose mambo mengi yatakayofuata katika mtandao huu.