Monday, October 10, 2016

UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA
Screenshot
Kutayarisha shambaShamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa mazao mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage). Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha sesa kinaweza kulimwa kwa kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha matuta kukinga mteremko kinafaa na kinapendekezwa kwa maeneo yenye mwinuko. Vilevile kilimo cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.
Screenshot-
MbeguNi muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa mtaalam aliyekaribu naye kabla ya kuamua kulima soya.
Aidha, mkulima anashauriwa kununua na kutumia mbegu kutoka katika sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano wa sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala wa mbegu, mashamba ya mbegu na vituo vya utafiti. Hii ni kwa sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji katika msimu mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota.
Kama mkulima hana uhakika na chanzo cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo ya uotaji (germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni kuzilowesha mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali penye joto la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka zitakapoota. Hesabu mbegu zilizoota na iwapo mbegu zilizoota ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani asilimia 75, mkulima anashauriwa kutopanda mbegu hizo.
Wakati wa kupandaUpandaji wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa aina za soya zinazokomaa mapema, soya ikipandwa mwanzoni mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa kipindi kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha na hivyo kufanya uvunaji na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu zitaoza au kuanza kuota na kupoteza ubora wake.
Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya kulingana na mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa soya inakomaa wakati hakuna mvua ili kurahisisha uvunaji na soya kutooza.
Jedwali linaonyesha mahali, aina na muda wa kupanda soya.
  Screenshot0
Nafasi ya kupandaMkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa na wataalamu. Nafasi hizo ni sentimeta 10 kwa sentimita 45 kwa soya fupi kama bossier na kwenye sehemu zenye rutuba hafi fu. Aidha, tumia sentimeta 10 kwa sentimita 60 kwa soya ndefu kama Uyole Soya 1 na kwenye sehemu zenye rutuba nyingi. Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa kina cha sentimeta mbili hadi sentimita tano ili zisiharibiwe au kuliwa na wanyama kama panya. Mkulima ahakikishe kuwa soya inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya kabla ya kupanda.

PaliziSoya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza isihitajike ambapo soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa imekua na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya pili kutohitajika. Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata hivyo inafaa kufuata
WADUDU, MAGONJWA NA WANYAMA WAHARIBIFU
Wadudu

Kwa sasa, nchini Tanzania soya haishambuliwi sana na wadudu kama ilivyo sehemu nyingine ambako zao hilo hulimwa kwa wingi. Hata hivyo endapo wadudu watatokea mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion 50% EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu kwenye mazao.
Tofauti na mazao kama mahindi na maharage, hakuna wadudu waharibifu wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza kutunzwa kwa muda mrefu ghalani bila kuwa na athari za wadudu. Kwa mkulima na wafanyabiashara, kutokuwepo wadudu waharibifu ghalani kunapunguza gharama za utunzaji hadi bei nzuri itakapofi kiwa.
Magonjwa
Kama ilivyo kwa wadudu, magonjwa ya soya ni machache. Hata hivyo magonjwa ambayo hutokea kwa nadra ni yale yanayotokana na vimelea vya ukungu na bakteria. Magonjwa hayo huenezwa kwa mbegu, masalia ya mimea shambani na wadudu mafuta. Hivyo ni bora kwa mkulima kuzingatia kanuni za kilimo bora au kupata ushauri wa kitaalamu ili kuepukana na magonjwa hayo. Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa katika zao la soya ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali husika.
Aidha, panda kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia mazao yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya kama alizeti na mahindi. Wanyama waharibifu Kwa kawaida soya hupendwa sana na panya wa shambani na ghalani. Wanyama wengine ni pamoja na sungura, paa, swala, n.k. Mkulima anashauriwa kutumia mbinu na njia mbalimbali zikiwemo za asili, kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu mazingira.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi usikose sehemu itakayofuata ya somo hili.

No comments:

Post a Comment