Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze usindikaji wa vitunguuu (Chachandu ya vitunguu (Onion mamaled))
Hii ni aina ya chachandu inayosindikwa kutokana na vitunguu. Chachandu hii ni kwa ajili ya kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na kuongeza hamu ya kula kwa watu wenye matatizo ya hamu ya kula.
Dondoo: Kiwango cha mahitaji yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya, kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 12 za ujazo wa nusu (½) lita.
Mahitaji
- Vitunguu maji kilo 5
- Vinega lita 3
- Sukari kilo 3
- Karawei kijiko 1 cha chai
- Karafuu, punje 12
- Chumvi vijiko 10 vya chakula
Maandalizi
- Menya vitunguu kuondoa maganda
- Osha kwa maji safi
- Katakata kwa muundo wa viboksi vidogo vidogo
- Andaa sufuria safi
- Weka vitunguu kisha uchanganye na chumvi
- Funika kwa muda wa saa moja
- Osha vitunguu hivyo kwa maji safi ya baridi mara tatu
- Chuja ili kuondoa maji yote
Kutengeneza
- Bandika sufuria jikoni
- Weka vitunguu ulivyokwisha kuosha
- Weka lita 3 za vinega
- Changanya sukari kilo 3
- Weka karawei kijiko kimoja cha chakula
- Weka punje 12 za karafuu ulizokuwa umeandaa
- Koroga taratibu ikiwa jikoni kwa muda wa saa 3 bila kuacha
Kufungasha
- Weka kwenye vifungashio ikiwa bado ya moto
- Funga vifuniko kiasi
- Tumbukiza kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea chenye maji ya moto kwa muda wa dakika 5
- Ondoa kisha ufunge vizuri
- Weka lebo tayari kwa kuuza
Baada ya matengenezo inashauriwa kupelekwa sokoni baada ya wiki moja.
Mamaled ya vitunguu inaweza kuliwa na chakula cha aina yoyote ili kuongeza ladha au hamu ya kula.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi.
No comments:
Post a Comment