HISTORIA YA
MAISHA YA MWALIMU NYERERE
KABLA YA UHURU
Wakati taifa linaadhimisha miaka 17 ya kifo cha mwasisi wa taifa, na rais wa kwanza wa Tanzania, kizazi kinahitaji kujua huyo alikuwa mtu gani na alianzia wapi.
Katika makala haya, tutaangalia sehemu tu ya historia ya mwalimu, nia ni kutaka kumuenzi na kujikumbusha kama huyu tunayemuenzi leo alikuwa mtu gani na jinsi alivyoishi.
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, Aprili 1922, katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara Tanzania (wakati ule Tanganyika). Alikuwa moja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.
Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
Kutokana na ujasiri na uelewa wake wa mambo mengi, Mapadre wa Kanisa Katoliki wakaona akili yake na nia yake nzuri ya kutaka kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943-1945. Akiwa katika Chuo cha Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia alijihusisha na uundwaji wa tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s).
Mwaka 1949 alipata ufadhili (Scholarship) ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti Uingereza akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.
Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari). Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.
Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.
Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961.
BAADA YA UHURU.
Baada ya uhuru Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.
Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
BAADA YA KUSTAAFU.
Baada ya kustaafu kazi ya ukuu wa nchi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la mahindi. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Foundation”, mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.
Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara baadaya alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.
Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu ( leukemia), iliyosababisha mauti yake.
MAFANIKIO YAKE
Ø Kujenga umoja wa Taifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili.
Ø Kushinda ubaguzi wa rangi, na juhudi zake kuchangia Taifa la Afrika kusini huru.
Ø Kutetea usalama wa taifa katika vita vya kagera dhidi ya Nduli Iddi Amin.
Ø Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini mwa Afrika, kama; Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia(SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).
CHANGAMOTO
Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa, na yeye kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais. Na kuruhusu kufanyika uchaguzi mwaka 1985, uchaguzi ambao ulimsimamisha Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais, ambaye alitawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.
SIFA ZAKE
Pamoja na changamoto na matatizo;
Ø Mwalimu kamwe hawezi kusahaulika kwa juhudi zake za kujenga umoja na mshikamano kwa watanzania, ambao ndio msingi wa amani tunayojivunia sasa.
Ø Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.
Ø Pia ataendelea kukumbukwa barani Afrika, hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ø Mwalimu ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwake miaka zaidi ya 24.
Ø Mwalimu ni mfano wa kuigwa kama kiongozi aliyefuata misingi ya maadili ya uongozi
na mzalendo wa nchi hii.
Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama.
Tarehe 14 Oktoba, 1999 mauti yalimkuta, kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu (Leukemia). Alizikwa sehemu alikozaliwa kijijini Butiama, mkoa wa Mara Mashariki mwa ziwa Victoria. Mwalimu aliacha mjane, watoto na wajukuu.

No comments:
Post a Comment