Saturday, October 29, 2016

ONGEZA PATO KWA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA(PEANUT BUTTER)

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga.
Image result for peanut butter

Mara nyingi, ni vizuri kuwaza kuwa kila zao unalozalisha unawezaje kuliboresha na kukupatia kipato zaidi. Wakulima wa karanga walio wengi wamezoea tu kulima na kuuza karanga mara baada ya kuvuna na kuwaacha wengine wasio wakulima wakifaidika zaidi kutokana na jasho lao.

Ni vizuri kutafuta na kujifunza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia kuboresha uzalishaji wako na pato likawa la uhakika zaidi, ambapo badala ya kuuza karanga zikiwa mbichi. Unaweza kutengeneza siagi ya karanga ukauza ikiwa bidhaa kamili.

Namna ya kutengeneza siagi ya karanga “Peanut butter”

  1. Chambua karanga kuhakikisha zote ni nzuri.
  2. Kaanga, menya na upepete.
  3. Pima uzito kisha saga mpaka ziwe laini.
  4. Andaa sukari, chumvi na mafuta ya alizeti.
  5. Mafuta yawe 20% ya uzito wa karanga, sukari 6% na chumvi 1.7%.
  6. Anza kuweka sukari na chumvi huku ukiongeza mafuta kidogo kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
  7. Bandika jikoni moto ukiwa kidogo kwa muda wa dakika kumi na tano.
  8. Baada ya muda huo weka kwenye vifungashio na kuweka nembo tayari kwa kupeleka sokoni.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga.

3 comments:

  1. Asante sana,i hope nitaendelea kujifunza mengi zaidi kupitia blog hii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu sana na asante kwakututembelea kwenye mtandaao wetu

      Delete
    2. Siagi hii inauwezo wakukaa mda gani bila kuharibika boss

      Delete