Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze namna ya kutengeneza mango pickle (achali ya embe)MANGO PICKLES au "ACHARI YA EMBE" ni chachandu inayo tumika kunogesha utamu wa chakula. Malighafi kuu katika utengenezaji wa "MANGO PICKLES " ni embe
Maitaji
- Nunua embe mbichi kabisa
- Chumvi
- Pilipili ya unga
- Nyanya
- Vitunguu na karot
- Pilipili mtama na iriki kama ukipenda inukie
- kitunguu saum
KUTENGENEZA
- Bandika sufuria yako jikoni iwe kwenye moto weka mafuta ya kula kaanga vitunguu
- Kisha kitunguu saum, weka karot, hoho kaanga
- Kisha nyanya wakati huo ulishaandaa maembe kwa kuyakata vipande upendavyo ila vidogo vinapendeza changanya na pilipili ya unga na chumvi vijiko viwili changanya peke ake pembeni weka chuja maji mana huwa vinatoaga maji hakikisha vimechanganyika vizuri na pilipili.
- Kisha vitose kwenye lost yako mpaka viive tayari kwa kuuzwa vipaki kwenye vikopo.
Hapa tunatengeza kwa ajili ya biashara na huwa inakaa miezi 3 hadi 6
ISIYOPIKWA
Mahitaji:
- embe
- vinager
- mafuta ya alizeti aldari
- uwatu
- pilipili masala
- vifungashio Lebo na sili.
KUANDAA
Jinsi ya kuandaa sasa ili iende sokon.
- Embe mbichi kabisa iwe dodo au tanga osha embe na katakata vipande vidogo saizi ya wastani hakikisha umeoshaa na maji safi na salama.
- Chukua ndoo weka vipande vya embe changanya na chunvi funika acha siku 5/21
- Baada ya hapo utachukua embe zako na kuziosha tena ili kupunguza chumvi.
- Baada ya hapo changanya kwa pamoja kisha jaza kwenye chupa sindilia vema ktk chupa ili kusiingie hewa na pia wakati unandaa zingatia usafi wa mikono na vitendea kazi hili la muhimu sana
- ukumaliza chukua mafuta ya alizeti pasha moto kisha utakuwa unaweka vijiko 2 pale juu ya mango pickle yako usijaze chupa ili kulinda bidhaa yako isiharibiki ukimaliza chukua chupa zako weka lebo na sili. Hapo zinakuwa Hapo zinakuwa tayari peleka sokoni
NB: Hii haipikwi tuelewane
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu achali ya embe.
Habari asante kwa somo nilikuwa nauliza sodium unaweza kutumia nasikia huwa inasaidia bidhaa isialibike he in sahihi nahitaju kufahamu
ReplyDeleteKitugani hutumika ili hio achari isiharibuke?
ReplyDelete