Tuesday, October 25, 2016

USINDIKAJI WA NYANYA (Chachandu ya Nyanya (Stewed tomato))

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo katika matandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze USINDIKAJI WA NYANYA (Chachandu ya Nyanya (Stewed tomato))
Wakulima hupata hasara kubwa sana inayotokana na mazao hayo kuharibika haraka kutokana na uhaba wa soko.

Uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali nchini Tanzania, na kwingineko, umeshika kasi sana kutokana na jitihada zinazofanywa na wakulima katika kuongeza uzalishaji huo.

Hili ni jambo muhimu sana kwa kuwa walaji wanatoshelezwa bila kupata taabu, huku wakulima nao wakipiga hatua kadhaa za kimaendeleo.

Juhudi hizi zinakatishwa tama na ukosefu wa soko la haraka la mboga mboga na matunda, huku wakulima wakiwa hawana namna ya kuhifadhi mazao hayo kwa lengo la kusubiri soko au kwa matumizi ya baadHii ni aina ya kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na hamu ya kula.ae. Wakulima huacha mazao hayo yakioza ovyo, na baada ya kuoza wakulima wanakata tamaa kwa kuwa hupata hasara kubwa kutokana na upotevu huo.

Ni muhimu kwa wakulima na Wajasiriamali kufahamu namna mbalimbali wanavyoweza kuhifadhi na kusindika mazao wanayozalisha, ili wasiingie katika hasara isiyokuwa ya lazima.

Kwa kufahamu hilo, nimewaletea somo la namna ya usindikaji waChachandu ya Nyanya (Stewed tomato))
Hii ni aina ya kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na hamu ya kula.
 
 
image
Namna ya kusindika chachandu ya nyanya Dondoo: Kiwango cha mahitaji yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 12 za nusu (½) lita.

Mahitaji

  1. Nyanya sadoline 2
  2. Pilipili hoho kilo 2
  3. Vitunguu maji kilo 1¼
  4. Chumvi vijiko 2 vya chai
Namna ya kuandaa
  1. Osha nyanya na pilipili hoho vizu kwa maji safi
  2. Menya vitunguu vizuri
  3. Katakata vyote kwa muundo wa viboksi vidogo vidogo
  4. Weka kwenye sufuria
  5. Bandika jikoni
  6. Koroga taratibu kwa muda wa nusu saa ili mchanganyiko huo usiungue
Ufungashaji
  1. Wakati mchanganyiko ukiendelea kuiva jikoni, hakikisha unaandaa vifungashio/chupa
  2. Ni muhimu kuhakikisha kuwa chupa hizo zimeoshwa vizuri na kuwekwa kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea (Sterilizer)
  3. Weka mchanganyiko wa chachandu kwenye vifungashio kulingana na ujazo unaohitaji ukiwa bado wa moto
  4. Funga chupa/kifungashio kiasi
  5. Rudisha kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea
  6. Acha humo kwa muda wa dakika tano
  7. Ondoa na ufunge vizuri
  8. Pindua chupa/kifungashio mfuniko ukae chini. Hii itasaidia mfuniko kufunga vizuri
  9. Weka nembo tayari kwa mauzo
Inashauriwa kuanza kuuza bidhaa hiyo baada ya wiki moja tangu siku ilipotengenezwa. Bidhaa hii inaweza kuwa salama kwa matumizi ya binadamu kwa kipindi cha miaka 2 tangu ilipotengenezwa.

Soko
Bidhaa hii inauzwa na kutumiwa na watu wa kada mbalimbali. Inaweza kuuzwa katika hoteli za kawaida na zile za kitalii, pamoja na maduka ya kawaida ya vyakula vya binadamu.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi juu ya usindikaji wa nyanya.

1 comment:

  1. Nimefurahi kupata elimu hii ambayo ni fursa ya wazi kwa wajasiriamali.

    ReplyDelete