Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo katika tujifunze jinsi ya KUVUNA, KUPURA NA KUHIFADHI SOYA.
Kuvuna Soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji wa shamba. Kwa mfano soya aina ya Bossier huchukua miezi mitatu hadi minne kukomaa na aina ya Uyole Soya 1 miezi minne hadi mitano. Dalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya njano.
Anza kuvuna baada ya majani kuanza kupukutika. Soya ikikauka, maganda yake hupasuka na mbegu hupukutikia chini. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi kuvuna soya mara inapokomaa na kuanza kukauka. Ili kuzuia upotevu wa zao shambani, inashauriwa kuvuna majira ya asubuhi au majira ambayo sio ya jua kali endapo soya imekauka na kuanza kupasuka wakati wa kuvuna. Kupura Soya haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu zake hupasuka kirahisi. Mara baada ya kupura, ondoa takataka na uchafu mwingine kwenye soya kwa kupepeta na kupembua. Kausha soya kufi kia wastani wa asilimia 10 ya kiasi cha maji (moisture moisture content content) kisha ihifadhi ghalani kwa matumizi au kusubiri soko.
Kuhifadhi
Hifadhi soya baada ya kuhakikisha kuwa imekauka vizuri. Ni muhimu kuhifadhi soya mahali pakavu ili soya isipate uvundo na kuharibu soya ya mbegu na ya chakula. Soya inaweza kuhifadhiwa kwenye vihenge au kwenye magunia kama mazao mengine, tofauti ni kutohitajika dawa ya kuhifadhia.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi usikose sehemu itakayofuata ya somo hili.
No comments:
Post a Comment