Wednesday, October 12, 2016

MAVUNO NA MAPATO YATOKANAYO NA ZAO LA SOYA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo katika sehemu ya mwisho wa zapo la SOYA tujifunze MAVUNO NA MAPATO YATOKANAYO NA ZAO LA SOYA

Mavuno
Soya ina uwezo wa kutoa kilo 1,500 hadi 2,500 kwa hekta kutegemea na aina, hali ya hewa, rutuba ya udongo, matumizi ya mbolea na utunzaji kuanzia wakati wa kuchagua mbegu, kulima, kupanda na kuvuna. Kiasi hicho cha mavuno ni sawa na kilo 600 hadi 1,000 kwa ekari moja.
Mapato Kutokana na mavuno ya soya, mkulima anaweza kupata mapato mengi ukilinganisha na mazao kama mahindi na maharage kwa eneo lililosawa na eneo la soya.
Ukweli huu unabainishwa na tathmini iliyofanyika mwaka wa 2005 na Wizara ya Kilimo na Chakula, juu ya hali kilimo cha soya nchini. Tathmini hiyo ilionyesha kuwa wastani wa gharama za kuzalisha kilo moja ya soya kwa mikoa ya Nyanda za Juu za Kusini hususan Songea Vijijini ni shilingi 130, kwa hiyo kama mkulima atauza soya kwa wastani wa shilingi mia mbili (200) kwa kilo moja bila gharama ya kusafi risha mbali na kijijini kwake anaweza kupata faida ya kati ya shilingi 105,000 hadi 175,000 kwa hekta moja au kati ya shilingi 42,000 na 70,000 kwa ekari moja.
Hata hivyo mapato yanaweza kuongezeka endapo mkulima atatunza na kuuza soya wakati bei imepanda kwa kuwa soya inaweza kutunzwa muda mrefu bila kuharibiwa na wadudu. Ni dhahiri kuwa zao la soya linaweza kumuongezea mkulima kipato na kumuondolea umaskini.
Screenshot-8.png
Screenshot-9.png

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu zao la SOYA kuanzia siku ya kwanza mpaka leo usikose mfululizi wa mafunzo mengi yatakayofuata kupitia mtandao huu.

No comments:

Post a Comment