Sunday, October 30, 2016

JE WALIJUA TUNDA AINA YA PAPAI?

Hujambo rafiki? 
Image result for papaya fruit

Tunda aina ya papai lina kiwango kikubwa cha vitamin C ikilinganishwa na chungwa, ulaji wa papai husaidia kuondoa sumu mwilini na kuimarisha kinga ya mwili.


Asante sana kwa kututembelea.

MALEZI YA VIFARANGA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze malezi ya vifaranga.
Wafugaji wengi wa kuku wanakubwa na changamoto nyingi katika ufugaji wa kuku (magonjwa ikiwa moja wapo) hasa hasa katika hatua za awali yani katika hatua ya kifaranga kwani katika ukuaji wa vifaranga ndicho kipindi ambaacho magonjwa mengi hunyemelea vifaranga, basi leo tutajifunza namna ya kuwachanja, ukifuatilia chanjo hizi unauwezo wa kukuza vifaranga wako kwa 99%.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKKMK5WQyUtd39LB83gdLgj9sAMBP1fMppsb-JsytYG8xK9ML8Syf9DFlz0sIkmgTf2cL7OafRgSijXzqiItopIpP5oN-cels2KKMCydng45o-wEmGxO3hYGcTKNFY_hZRlfG9LQWysIw/s640/150304100318_chick_sexing_gch_pair_640x360_afp_nocredit.jpg
MALEZI YA VIFARANGA.
SIKU 1-5—
:
VITEX,FLUBANA,OTS PLUS,TEYPHOPRIM,TRIMAZIN,TETRACLOVIT,SUPER CHICKPLUS

SIKU YA 7—: CHANJO YA KIDERI (BAADA YA HAPO MAJI YA VITAMINI)
SIKU YA 8-12—: TYLODOX,FLUEBAN, AMPRILIUM + VITAMIN
WIKI YA 2—: GOMBOLO
WIKI YA 3—: VITOX,AMPROLIUM,DOXCOLTRIMOZIN, OTC 20%, ESB3
WIKI YA 4—: DAWA YA MINYOO
WIKI YA 5—: VITAMINI
WIKI YA 8—: CHANJO YA NDUI (SINDANO), DAWA YA MINYOO(WALE GROWERS)
WIKI YA 12—: CHANJO YA KIDERI * TYPHOD(SINDANO)
WIKI YA 16—: KUKU WALISHWE LAYERS NOLASES
WIKI YA 48—: KUCHAMBUA KUKU

Ukizingatia chanjo hii na mpangilio wa chakula kwa kuku huwezi kumpoteza kifaranga hata mmoja labda kwa kitu kingine lakini sio kwa ugojwa.
Chanjo ni muhimu sana katika kuku kwani huwaongezea kinga dhidi ya magojwa ambayo yangewashambulia.

NB—: Usiwape chanjo kuku kama wameshaonyesha dalili za magojwa kama vile kideri au ndui kwasababu utawaua wote, ni vyema kama umeona dalili hizi kwa kuku wako ukawapa anti biotics ili kupunguza uwezekano wa kupatwa na magojwa mwengine nyemelezi.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza  juu ya malezi ya vifaranga ili kuboresha ufugaji wako.

Saturday, October 29, 2016

ONGEZA PATO KWA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA(PEANUT BUTTER)

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga.
Image result for peanut butter

Mara nyingi, ni vizuri kuwaza kuwa kila zao unalozalisha unawezaje kuliboresha na kukupatia kipato zaidi. Wakulima wa karanga walio wengi wamezoea tu kulima na kuuza karanga mara baada ya kuvuna na kuwaacha wengine wasio wakulima wakifaidika zaidi kutokana na jasho lao.

Ni vizuri kutafuta na kujifunza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia kuboresha uzalishaji wako na pato likawa la uhakika zaidi, ambapo badala ya kuuza karanga zikiwa mbichi. Unaweza kutengeneza siagi ya karanga ukauza ikiwa bidhaa kamili.

Namna ya kutengeneza siagi ya karanga “Peanut butter”

  1. Chambua karanga kuhakikisha zote ni nzuri.
  2. Kaanga, menya na upepete.
  3. Pima uzito kisha saga mpaka ziwe laini.
  4. Andaa sukari, chumvi na mafuta ya alizeti.
  5. Mafuta yawe 20% ya uzito wa karanga, sukari 6% na chumvi 1.7%.
  6. Anza kuweka sukari na chumvi huku ukiongeza mafuta kidogo kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
  7. Bandika jikoni moto ukiwa kidogo kwa muda wa dakika kumi na tano.
  8. Baada ya muda huo weka kwenye vifungashio na kuweka nembo tayari kwa kupeleka sokoni.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga.

Friday, October 28, 2016

ELIMU YA UWEKEZAJI

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze juu ya ELIMU YA UWEKEZA

UWEKEZAJI NI NINI?UWEKEZAJI ni njia ya kufanya fedha zako kuzaa fedha zaidi. Ili uweze kuwa mwekezaji   unapaswa kuwa na shughuli inayokuingizia kipato kwanza halafu ndipo unaweza kuwekeza sehemu ya kipato chako ambacho kinaweza kutokana na mshahara, kufanya biashara na kadhalika.

ILI   UWEZE    KUWEKEZA     UNAPASWA   KUWEKA   AKIBA  SEHEMU   YA  MAPATO   YAKO . Tunaweza kuwa na hekima ya kuweka akiba  angalau asilimia (10%) ya mapato yako ya kila mwezi kwa lengo la kuwekeza, nidhamu hiyo inawafanya watu wengi kuwa matajiri.

FANYA    FEDHA   ZAKO   ZIKUFANYIE    KAZI  BADALA    YA   KUWA   MTUMWA    WA   FEDHA.
Moja kati ya mali (asset) zako muhimu unazo takiwa kuziendeleza ni uwezo wako wa kuzalisha kipato “your earning ability” hii ni mali (asset) muhimu sana ambayo inatakiwa kuendelezwa kila siku.
Watu wengi hii earning ability imekuwa dormant, haikui, wengine ndiyo inazidi kuporomoka, na hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha pato lao kuto kuongezeka.
Hii "earning ability" ni tofauti na fani yako, naomba usichanganye  hili, hii ni tofauti na fani yako kama uhasibu, udaktari, mwanasheria n.k, au ujuzi wako mwingine kama udereva, ufundi n.k
Watu wengi hawajui kutofautisha hili, wana develop fani zao, lakini hawa kuzi "earning ability" matokeo yake wanaweza wakawa vizuri sana kwenye taaluma zao, lakini  pato lao, ni dogo au liko pale pale halikuwi, kwanini? Fani yako na your earning ability ni vitu viwili tofauti, although vina relate.

Earning ability ni uwezo wa kuingiza kipato, hii ni skill tofauti unatakiwa kuiendeleza, watu wengi ability yao ya kuearn, iko kwenye eneo moja tu " profession zao" ndiyo maana income zao ziko very limited, ikitokea bahati mbaya akapata matatizo ajira ikasimama, basi maisha yanayumba kabisa. Hii ni kwasababu they haven't developed their earning ability nje ya ajira zao.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu.

Thursday, October 27, 2016

MAAJABU YA MMEA WA ALOE VERA (SHUBIRI MWITU) KWA KUKU

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze MAAJABU YA MMEA WA ALOE VERA (SHUBIRI MWITU) KWA KUKU.

Kuku ni moja ya miradi inayofanywa kwa wingi na watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wakulima na wafugaji, na wanaofanya shughuli nyinginezo.
Moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili na kuzungumziwa mara kwa mara ni magonjwa yanayoshambulia kuku, bila wafugaji kufahamu ni nini cha kufanya.

Kumekuwepo na njia mbalimbali za kutibu kuku, zikiwemo za asili na zisizokuwa za asili. Moja wapo ya tiba rahisi ya asili kwa kuku ni kwa kutumia shubiri mwitu maarufu kama Aloe Vera. Mmea ambao umekuwa ukisifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu, wanyama na ndege.
Shubiri mwitu mbali na kutibu kuku, hutumika pia kwa wanyama na binadamu.
ALOE VERA
Shubiri mwitu (Aloe) imekuwa ikitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeneza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka mkazo kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa mharo mwekundu na kwa kiasi fulani mdondo-Newcastle disease.
Tafiti zilizofanyika kwa kutumia mti huu kutibu ugonjwa wa mharo mwekundu-coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani. Maji maji ya mmea huu yana uwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia 50 dhidi ya maonjwa mbalimbali.

Kupanda
Mmea wa Aloe Vera unaweza kupandwa maeneo ya karibu na mabanda ya kuku ili kurahisisha upatikanaji wake na unakubali maeneo karibu yote.
images

Shubiri mwitu kwa ukuaji wa kuku.
Shubiri mwitu inapowekwa kwenye maji inasaidia kwa kiasi kikubwa kuku kukua haraka. Mililita 15 had 20 za maji ya shubiri mwitu yakichanganywa na lita tano za maji kila siku kwa kuku 90 yana uwezo wa kusaidia ukuaji wa kuku na kuongeza uzito ukilinganisha na wale ambao hawajapewa.

Uandaaji wa Shubiri mwitu Kunywa
Shubiri mwitu (moja) inaweza kukatwe vipande vipande na kulowekwa ndani ya maji ya kunywa kiasi cha lita 1-hadi 3 kutegemeana na idadi ya kuku. Viache vipande hivyo kwenye maji kwa siku kadhaa hadi unapobadilisha maji ndipo uviweke vingine. Ukiweza kuchuja mchuzi wa shubiri mwitu basi unakuwa ukitumia mililita 15 ndani ya lita tano ya maji ya kunywa kuku kwa kuku 90 kama una kuku wachache basi punguza kiasi cha dawa au ongeza kama ni wengi.
aloejuice1

Vidonda.
Kuku wenye vidonda kama ilivyo kwa ugonjwa wa mdondo (Newcastle Disease) inakubidi utengeneze unga. Kata vipande vidovidogo vya shubiri mwitu kisha changanya na pumba kidogo, vitwange na kuvichekecha ili upate unga laini.
Anika na kisha tunza vizuri tayari kwa kuutumia mara kuku wauguapo. Kuku wenye vidonda waoshwe vizuri kwa maji safi na sabuni pamoja na chumvi kidogo. Baada ya hapo paka unga wa shubiri kwenye vidonda hivyo.
Njia hii ya asili ni nzuri na muhimu sana kwa utunzaji wa kuku, kwa kuwa hupunguza uwezekano wa matumizian ya madawa makali ya viwandani ambayo yana madhara kwa walaji na mazingira.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi kuhusu shubiri kwa kuku.













Wednesday, October 26, 2016

USINDIKAJI WA VITUNGUU (Chachandu ya vitunguu (Onion mamaled))

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo kwenye mtandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze usindikaji wa vitunguuu (Chachandu ya vitunguu (Onion mamaled))


 image_thumb2
Hii ni aina ya chachandu inayosindikwa kutokana na vitunguu. Chachandu hii ni kwa ajili ya kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na kuongeza hamu ya kula kwa watu wenye matatizo ya hamu ya kula.
 
Dondoo: Kiwango cha mahitaji yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya, kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 12 za ujazo wa nusu (½) lita.
 
Mahitaji

  1. Vitunguu maji kilo 5
  2. Vinega lita 3
  3. Sukari kilo 3
  4. Karawei kijiko 1 cha chai
  5. Karafuu, punje 12
  6. Chumvi vijiko 10 vya chakula

Maandalizi

  1. Menya vitunguu kuondoa maganda
  2. Osha kwa maji safi
  3. Katakata kwa muundo wa viboksi vidogo vidogo
  4. Andaa sufuria safi
  5. Weka vitunguu kisha uchanganye na chumvi
  6. Funika kwa muda wa saa moja
  7. Osha vitunguu hivyo kwa maji safi ya baridi mara tatu
  8. Chuja ili kuondoa maji yote

Kutengeneza

  1. Bandika sufuria jikoni
  2. Weka vitunguu ulivyokwisha kuosha
  3. Weka lita 3 za vinega
  4. Changanya sukari kilo 3
  5. Weka karawei kijiko kimoja cha chakula
  6. Weka punje 12 za karafuu ulizokuwa umeandaa
  7. Koroga taratibu ikiwa jikoni kwa muda wa saa 3 bila kuacha

Kufungasha

  1. Weka kwenye vifungashio ikiwa bado ya moto
  2. Funga vifuniko kiasi
  3. Tumbukiza kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea chenye maji ya moto kwa muda wa dakika 5
  4. Ondoa kisha ufunge vizuri
  5. Weka lebo tayari kwa kuuza

Baada ya matengenezo inashauriwa kupelekwa sokoni baada ya wiki moja.

Mamaled ya vitunguu inaweza kuliwa na chakula cha aina yoyote ili kuongeza ladha au hamu ya kula.

 

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi.

Tuesday, October 25, 2016

USINDIKAJI WA NYANYA (Chachandu ya Nyanya (Stewed tomato))

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo katika matandao wetu wa zinduka sasa blog tujifunze USINDIKAJI WA NYANYA (Chachandu ya Nyanya (Stewed tomato))
Wakulima hupata hasara kubwa sana inayotokana na mazao hayo kuharibika haraka kutokana na uhaba wa soko.

Uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali nchini Tanzania, na kwingineko, umeshika kasi sana kutokana na jitihada zinazofanywa na wakulima katika kuongeza uzalishaji huo.

Hili ni jambo muhimu sana kwa kuwa walaji wanatoshelezwa bila kupata taabu, huku wakulima nao wakipiga hatua kadhaa za kimaendeleo.

Juhudi hizi zinakatishwa tama na ukosefu wa soko la haraka la mboga mboga na matunda, huku wakulima wakiwa hawana namna ya kuhifadhi mazao hayo kwa lengo la kusubiri soko au kwa matumizi ya baadHii ni aina ya kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na hamu ya kula.ae. Wakulima huacha mazao hayo yakioza ovyo, na baada ya kuoza wakulima wanakata tamaa kwa kuwa hupata hasara kubwa kutokana na upotevu huo.

Ni muhimu kwa wakulima na Wajasiriamali kufahamu namna mbalimbali wanavyoweza kuhifadhi na kusindika mazao wanayozalisha, ili wasiingie katika hasara isiyokuwa ya lazima.

Kwa kufahamu hilo, nimewaletea somo la namna ya usindikaji waChachandu ya Nyanya (Stewed tomato))
Hii ni aina ya kiungo ambacho hutumika kuongeza ladha kwenye chakula, pamoja na hamu ya kula.
 
 
image
Namna ya kusindika chachandu ya nyanya Dondoo: Kiwango cha mahitaji yatakayoainishwa hapo chini na maelezo yake ni kwa ajili ya kutengeneza na kupata kiasi cha chupa 12 za nusu (½) lita.

Mahitaji

  1. Nyanya sadoline 2
  2. Pilipili hoho kilo 2
  3. Vitunguu maji kilo 1¼
  4. Chumvi vijiko 2 vya chai
Namna ya kuandaa
  1. Osha nyanya na pilipili hoho vizu kwa maji safi
  2. Menya vitunguu vizuri
  3. Katakata vyote kwa muundo wa viboksi vidogo vidogo
  4. Weka kwenye sufuria
  5. Bandika jikoni
  6. Koroga taratibu kwa muda wa nusu saa ili mchanganyiko huo usiungue
Ufungashaji
  1. Wakati mchanganyiko ukiendelea kuiva jikoni, hakikisha unaandaa vifungashio/chupa
  2. Ni muhimu kuhakikisha kuwa chupa hizo zimeoshwa vizuri na kuwekwa kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea (Sterilizer)
  3. Weka mchanganyiko wa chachandu kwenye vifungashio kulingana na ujazo unaohitaji ukiwa bado wa moto
  4. Funga chupa/kifungashio kiasi
  5. Rudisha kwenye chombo maalumu cha kuulia vimelea
  6. Acha humo kwa muda wa dakika tano
  7. Ondoa na ufunge vizuri
  8. Pindua chupa/kifungashio mfuniko ukae chini. Hii itasaidia mfuniko kufunga vizuri
  9. Weka nembo tayari kwa mauzo
Inashauriwa kuanza kuuza bidhaa hiyo baada ya wiki moja tangu siku ilipotengenezwa. Bidhaa hii inaweza kuwa salama kwa matumizi ya binadamu kwa kipindi cha miaka 2 tangu ilipotengenezwa.

Soko
Bidhaa hii inauzwa na kutumiwa na watu wa kada mbalimbali. Inaweza kuuzwa katika hoteli za kawaida na zile za kitalii, pamoja na maduka ya kawaida ya vyakula vya binadamu.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi juu ya usindikaji wa nyanya.

Monday, October 24, 2016

JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO.

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze namna Kutengeneza mafuta ya mgando(meupe)

Maitaji
  1. Micro wax kilo moja
  2. White oil Lita mbili
  3. Perfume vijiko viwili
Kutengeneza
  1. Chukua sufuria kavu bandika jikoni weka micro wax kilo moja
  2. Kisha white oil Lita mbili iache mpaka ichemke kwa muda mfupi utaweka perfume vijiko viwili mimina humo
  3. Baada ya hapo utaiacha ichemke kidogo kisha isikae sana ichemke mana italipuka kwahyo wakati unaipika moto uwe wa wastani kisha acha ipoe ibakie ya uvuguvugu
Mpaka hapo itakua imekamilika mgando wako weka lebo

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza JINSI YA KUTENGENEZA MAFUTA YA MGANDO

Sunday, October 23, 2016

KUVIMBA MWILI

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze kuhusu tatizo la KUVIMBA MWILI

Kuvimba uso, miguu, tumbo na shinikizo la damu ni dalili za ugonjwa wa figo. Uonapo hivyo wahi hospitali ukatibiwe kabla ya figo kushindwa kufanya kazi kabisa.


Asante sana kwa kuutembelea mtandao wetu.

Saturday, October 22, 2016

KUWASHWA MWILI

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze kuhusu KUWASHWA MWILI


Kuwashwa sehemu yoyote ya mwili ni matokeo ya tatizo fulani, kama vile minyoo, inaweza kuwa ni dalili za ugonjwa unaohitaji kuchunguzwa na kutibiwa.


Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu.

Friday, October 21, 2016

VISABABISHI VYA KWIKWI

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze VISABABISHI VYA KWIKWI
Visababishi vya Kwikwi: Kula kwa haraka chakula cha moto, Kulia au kukasirika, chakula chenye viungo vingi au pilipili, Kunywa pombe, au kupatwa na msituko.
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu.

Thursday, October 20, 2016

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ANAYETAPIKA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ANAYETAPIKA
Uonapo mtu anatapika, basi chemsha maji yenye tangawizi yapooze na umpe anywe, dalili zikizidi mwone daktari kwa msaada zaidi.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu.

Wednesday, October 19, 2016

DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI.

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI.
Kizunguzungu, kuishiwa nguvu na kuchoka haraka ni dalili za upungufu wa damu. Wahi hospitalini kwa uchunguzi.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi.

Tuesday, October 18, 2016

DALILI ZA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze DALILI ZA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI
Dalili za kuziba mirija ya uzazi kwa wanawake;
Ugumba, maumivu chini ya tumbo ya mara kwa mara na mimba kuharibika. Uonapo dalili mwone daktari kwa uchunguzi.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi.


Monday, October 17, 2016

NAMNA YA KULALA

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze NAMNA YA KULALA

Wakati mzuri wa kulala ni kuanzia saa nne hadi kumi usiku. Usilale mara tu baada ya kula chakula au kumeza dawa, vuta muda wa kupumzika kidogo.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza mengi.

Sunday, October 16, 2016

KUTENGENEZA LOTION

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze KUTENGENEZA LOTION
Maitaji
  1. Micro wax kilo moja na nusu
  2. White oil lita tatu
  3. Perfume vijiko viwili
KUTENGENEZA
Unawasha jiko kwa moto wa wastani unabandika sufuria yako
Kisha weka White oil kwenye sufuria ongeza na micro wax kilo moja n nusu
Baada ya hapo weka perfume vijiko viwili na uache ichemke kwa dakika kumi
Kisha ipua sufuria yako na kusubiri ipoe na kuanzia hapo unaweza kuiweka kwenye makopo tayari lotion kamili.

Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza JINSI YA KUTENGENEZA LOTION

Saturday, October 15, 2016

JINSI YA KUANDAA JUISI YA MAKAKALA AU PASHEN.

Hujambo rafiki karibu sana siku hii ya leo tujifunze JINSI YA KUANDAA JUISI YA MAKAKALA AU PASHEN.
MAHITAJI
  1. Pashen ndoo moja kubwa
  2. Sukari nyeupe
  3. kisu
  4. maji safi yaliyochemshwa
  5. sufuria
  6. blender
  7. chujio,
  8. mwiko
  9. Jiko la mkaa .
JINSI YA KUANDAA
  1. Osha mikono kwa sabuni na maji safi kwa ajili ya kuandaa juisi yako.
  2. Chukua pashen zako osha na maji safi na wakati huo angalia pashen mbovu usitumie hakikisha pashen ni zile zilizoiva vizuri na si mbovu.
  3. Kata pashen na toa zile mbegu za ndani baada ya kutoa mbegu chukua blender yako na saga pashen bila kuongeza kitu chchote na baada ya hapo chuja upate juisi.
  4. Baada ya hapo chukua sufuria safi weka juisi yako
  5. Kabla ya hapo pima juisi kupata uhakika unapika juisi ya kiasi gani hapo ieleweke tunatumia uwiyano sawa juisi.
  6. Kama ni vikombe 5 na sukari vikombe 5 koroga mpk sukari iyeyuke Dk15 baada ya hapo weka jikoni na uanze kukoroga mara moja mpka juisi iive ndani ya dk 25/30na usiache kukoroga mpk iive ili kutambua juisi km imeivaa itachemka na kutoa povu mwisho povu litapotea kabisa ipua na weka kwenye sufuria ya maji ambayo itadumbukia robo 3 ya sufuria uliyopikia juisi
  7. Hakikisha juisi imepoa vema kabla hujapaki kwenye vifungashio.
NB. Ili juisi yako iwe safi zingatia usafi na kanuni za usafi kwenye vitu hivyo na juisi ikipoa weka kwenye chupa na juisi hiyo huwa inauwezo wa kudumu kwa miezi 6 hadi 12
Asante sana kwa kuutembelea mtandao huu na kujifunza JINSI YA KUANDAA JUISI YA MAKAKALA AU PASHEN.

Friday, October 14, 2016

HISTORIA YA MAISHA YA MWALIMU NYERERE

HISTORIA YA MAISHA YA MWALIMU NYERERE

KABLA YA UHURU

Wakati taifa linaadhimisha miaka 17 ya kifo cha mwasisi wa taifa, na rais wa kwanza wa Tanzania, kizazi kinahitaji kujua huyo alikuwa mtu gani na alianzia wapi.

Katika makala haya, tutaangalia sehemu tu ya historia ya mwalimu, nia ni kutaka kumuenzi na kujikumbusha kama huyu tunayemuenzi leo alikuwa mtu gani na jinsi alivyoishi.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, Aprili 1922, katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara Tanzania (wakati ule Tanganyika). Alikuwa moja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.

Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Kutokana na ujasiri na uelewa wake wa mambo mengi, Mapadre wa Kanisa Katoliki wakaona akili yake na nia yake nzuri ya kutaka kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943-1945. Akiwa katika Chuo cha Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia alijihusisha na uundwaji wa tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s).

Mwaka 1949 alipata ufadhili (Scholarship) ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti Uingereza akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari). Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961.

BAADA YA UHURU.
Baada ya uhuru Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.
Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

BAADA YA KUSTAAFU.
Baada ya kustaafu kazi ya ukuu wa nchi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la mahindi. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Foundation”, mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara baadaya alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.
Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu ( leukemia), iliyosababisha mauti yake.

MAFANIKIO YAKE
Ø Kujenga umoja wa Taifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili.
Ø Kushinda ubaguzi wa rangi, na juhudi zake kuchangia Taifa la Afrika kusini huru.
Ø Kutetea usalama wa taifa katika vita vya kagera dhidi ya Nduli Iddi Amin.
Ø Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini mwa Afrika, kama; Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia(SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).

CHANGAMOTO
Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa, na yeye kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais. Na kuruhusu kufanyika uchaguzi mwaka 1985, uchaguzi ambao ulimsimamisha  Ali Hassan Mwinyi  kuwa Rais, ambaye alitawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.

SIFA ZAKE           
Pamoja na changamoto na matatizo;
Ø Mwalimu kamwe hawezi kusahaulika kwa  juhudi zake za kujenga umoja na mshikamano kwa watanzania, ambao ndio msingi wa amani tunayojivunia sasa.
Ø Bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.
Ø Pia ataendelea kukumbukwa barani Afrika, hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ø Mwalimu ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwake  miaka zaidi ya 24.
Ø Mwalimu ni mfano wa kuigwa kama kiongozi aliyefuata misingi ya maadili ya uongozi
na mzalendo wa nchi hii.

Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama.
 

Tarehe 14 Oktoba, 1999 mauti yalimkuta, kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu (Leukemia). Alizikwa sehemu alikozaliwa kijijini Butiama, mkoa wa Mara Mashariki mwa ziwa Victoria. Mwalimu aliacha mjane, watoto na wajukuu.